Kiswahili na Maendeleo Mashambani nchini Kenya

Makala hii inatathmini umuhimu wa lugha ya Kiswahili katika kuchangia maendeleo nchini Kenya. Haya hutokea kwa awamu ya muda mrefu. Maendeleo kwa jumla humaanisha mabadiliko chanya ya mwanadamu katika harakati zake zote za kimaisha. Maendeleo ni lazima kwa mwanadamu duniani. Hakuna wanadamu wanaobaki jinsi walivyo miaka nenda miaka rudi. Kuna maendeleo ya kibinafsi na ya kijamii. Yote haya huwezeshwa na kiwango cha uchumi. Uchumi hukua kutokana na uzalishaji mali. Uzalishaji mali hutokea katika mashamba na mitambo au viwanda. Uwezo huu huletwa na jamii kujifunza mbinu na stadi za uzalishaji mali. Mtu anapojifunza stadi fulani, lazima atumie lugha anayoielewa. Kwa hivyo, stadi hazikuzwi kwa Kiingereza bali lugha yoyote ile. Nchi nyingi ulimwenguni hazitumii Kiingereza na zimeendelea sana, mfano Ujerumani, Ufaransa, Italia, Malasyia, Korea Kisini na kadhalika. Kwa hivyo, tunahoji, je, Kiswahili kinaweza kutumiwa kujifunza mbinu na stadi mbalimbali za kuzalisha mali nchini Kenya? Hali hiyo inatokana na sababu kwamba Kiswahili ni somo la lazima nchini kutoka shule za msingi hadi shule za sekondari. Aidha, ni lugha rasmi na ya taifa. Hivyo ni lingua franka nchini. Kwa kurejelea ithibibati iliyopatikana nchini Kenya, makala hii inatalii dhima ya Kiswahili katika maendeleo kwenye maeneo ya mashambani.
JIUNGE NASI ILI KUPOKEA MACHAPISHO KWENYE BARUA PEPE

Jarida hili hutokea mara moja kwa mwaka (Novemba) na huchapisha makala ambazo hazijawahi kuchapishwa katika taaluma ya Lugha, Isimu na Fasihi ya Kiswahili na lugha nyingine za Kiafrika. Makala yasiyozingatia masharti yaliyowekwa na wahariri hayawezi kuchapishwa.