Matumizi ya Teknohama na Lugha ya Kiswahili kama Nyenzo ya Kuendeleza Sekta ya Kilimo: Tathmini ya Majukwaa ya Youtube na Facebook

Ulimwengu wa sasa umeshuhudia athari chanya na hasi katika matumizi ya teknolojia. Kwa hakika, karibu kila eneo la maisha ya binadamu katika ulimwengu wa sasa linashuhudia matumizi ya aina mbalimbali za teknolojia katika sekta mbalimbali, iwe elimu, biashara na kilimo kwa lengo la kufikia malengo ya Maendeleo Endelevu. Haya ni malengo ya matamanio ya ulimwengu yanayokusudiwa kuleta maendeleo ya kiuchumi, ujumuishwaji wa kijamii na uendelevu wa mazingira. Mojawapo ya malengo ya maendeleo endelevu ni kutokomeza njaa, kuwa na uhakika wa chakula, lishe bora na kukuza kilimo endelevu. Ili kufikia lengo hili, ni muhimu kilimo kiboreshwe, kikuzwe na kiwe endelevu ili ifikiapo 2030 tatizo la njaa liwe limekwisha. Vivyo hivvo, ni muhimu kuwashirikisha wakulima kupitia njia za mawasiliano zinazopatikana kwa urahisi na zinazoeleweka. Lugha ya Kiswahili ina jukumu la kutekeleza mawasiliano miongoni mwa wakulima kwa kuwa ni lugha inayowafikia watu wengi Afrika Mashariki. Katika enzi hii, nyenzo za kuwafikia wakulima hazina budi kuhusisha TEKNOHAMA. Ni katika muktadha huu ambapo makala hii inalenga kutathmini mitandao ya kijamii, hasusan YouTube na Facebook, kwa kubainisha aina ya ushauri unaotolewa kwa wakulima na upokezi wake pamoja na changamoto zozote wanazokumbana nazo. Hatimaye, mapendekezo kuhusu mikakati ya kukabiliana na changamoto hizo yametolewa.
JIUNGE NASI ILI KUPOKEA MACHAPISHO KWENYE BARUA PEPE

Jarida hili hutokea mara moja kwa mwaka (Novemba) na huchapisha makala ambazo hazijawahi kuchapishwa katika taaluma ya Lugha, Isimu na Fasihi ya Kiswahili na lugha nyingine za Kiafrika. Makala yasiyozingatia masharti yaliyowekwa na wahariri hayawezi kuchapishwa.