Sitiari katika Bembelezi za Watikuu

Lugha inayotumiwa katika utunzi wa nyimbo za watoto aghalabu huwa rahisi na hueleweka haraka. Pia huwa na urudiaji mwingi wa maneno katika mistari yake. Kuna aina nne za nyimbo za watoto: nyimbo za michezo, nyimbo za chekechea, nyimbo za dini za watoto na bembelezi. Tafiti za awali za nyimbo hizi zinaonyesha kuwa lugha inayotumiwa ni rahisi. Hata hivyo, bembelezi za Watikuu zinaonyesha ukiushi wa kaida zilizozoeleka za lugha katika nyimbo za watoto kwa kuwa zina urejelezi, kejeli na mafumbo chungu nzima ambayo ni kinyume cha sifa za lugha ya nyimbo za watoto. Sura hii inachanganua kipengele cha sitiari katika bembelezi hizo ili kutambua yaliyomo
JIUNGE NASI ILI KUPOKEA MACHAPISHO KWENYE BARUA PEPE

Jarida hili hutokea mara moja kwa mwaka (Novemba) na huchapisha makala ambazo hazijawahi kuchapishwa katika taaluma ya Lugha, Isimu na Fasihi ya Kiswahili na lugha nyingine za Kiafrika. Makala yasiyozingatia masharti yaliyowekwa na wahariri hayawezi kuchapishwa.