Ufupishaji kama Mkakati wa Uundaji wa Istilahi za Kiswahili zinazotumika katika Kompyuta

Teknolojia ya Kompyuta imepenyeza takriban kila kipengele cha maisha ya mwanadamu huku istilahi zikiwa kiungo cha kati katika mawasiliano ya kiufundi. Mojawapo ya sifa kuu zinazobainisha istilahi zilizoundwa kwa ufupisho ni maumbo yaliyopunguzwa kwa lengo la kufanikisha iktisadi. Kutokana na uhalisi huo, makala haya yamedhamiria kuchanganua mikakati ya ufupisho kama mbinu ya uundaji istilahi za Kiswahili kwenye medani ya Kompyuta. Kimsingi, huu ni utafiti wa maktabani. Sampuli ya vidahizo 69 viliteuliwa kwa uteuzi wa kudhamiria kutoka katika orodha ya vidahizo 3286 vya Kamusi Sanifu ya Kompyuta (Kiputiputi, 2011). Istilahi zilizokusanywa ziliainishwa katika makundi na kuchanganuliwa kwa utaratibu wa kithamano na kiwingidadi. Mikakati iliyotumiwa kuziunda istilahi hizo ndiyo iliyotathminiwa ili kubaini iwapo misingi ya kisayansi ya uundaji wa istilahi ya PEGITOSCA (Kiingi, 1989) imezingatiwa. Tumebainisha ufaafu wa istilahi za ufupisho zinazotumika katika Kompyuta. Hoja inayojengwa ni: je, istilahi za Kiswahili zinazotumika katika kompyuta zilizoundwa kwa ufupisho zina ufaafu?
JIUNGE NASI ILI KUPOKEA MACHAPISHO KWENYE BARUA PEPE

Jarida hili hutokea mara moja kwa mwaka (Novemba) na huchapisha makala ambazo hazijawahi kuchapishwa katika taaluma ya Lugha, Isimu na Fasihi ya Kiswahili na lugha nyingine za Kiafrika. Makala yasiyozingatia masharti yaliyowekwa na wahariri hayawezi kuchapishwa.